Kurudisha bidhaa na kurejeshewa pesa
Imesasishwa mwisho
Muda ulio nao
- Siku 7 tangu kupokea kwa bidhaa nyingi.
- Siku 15 tangu kupokea ikiwa bidhaa ina hitilafu.
Baadhi ya bidhaa haziwezi kurudishwa kwa sababu za usafi au usalama, kama vile nguo za ndani na bidhaa zinazoharibika haraka. Ukurasa wa bidhaa hueleza pale bidhaa isipoweza kurudishwa.
Jinsi ya kurudisha bidhaa
- Fungua oda kwenye akaunti yako na uombe kurudisha, ukitueleza sababu.
- Ikiwa bidhaa ilifika imeharibika au ina hitilafu, ongeza picha.
- Mkabidhi msafirishaji wetu atakapokuja kuichukua, au ipeleke kwenye kituo cha kuchukulia mizigo.
Kurejeshewa pesa
Tunakagua kila bidhaa iliyorudishwa kwenye kituo chetu na kukujulisha matokeo. Ikipita ukaguzi, tunakurejeshea pesa ndani ya siku 5 za kazi, kwa njia uliyolipia (M-Pesa au kadi) au kwenye Sotika Wallet yako.
Umebadili nia kabla ya kupokea?
Unaweza kughairi na kurejeshewa pesa zote hadi oda yako itakaposafirishwa.